Spika huyo amesema hayo Jumatatu wakati wa kikao cha bunge Dodoma.
“Kwa mamlaka niliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi sasa napiga marufuku wabunge wote wenye kope na kucha bandia kuingia Bungeni,” Ndugai amesema.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Tanzania, Spika ameongeza kuwa anashauriana na wataalamu kabla ya kufanya uamuzi iwapo aruhusu au asiruhusu wabunge wanaotumia vipodozi kupita kiasi kuingia katika Bunge.
Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndugulile kuliambia Bunge kuwa wanawake wanaotumia kucha na kope bandia wanakabiliwa na hatarisho kubwa la kiafya ambalo linaigharimu taifa.
Kwa mujibu wa ripoti za afya zilizo thibitishwa, sio chini ya wanawake 700 wanalazwa hospitali nchini Tanzania wakiwa wanasumbuliwa na athari za kutumia kope na makucha bandia na kujichubuwa.