Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 07:57

Somalia yataka mpango wa kuondoa vikosi vya kulinda amani kucheleweshwa


PICHA YA MAKTABA: Maafisa wa kikosi cha umoja wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia (ATMIS)
PICHA YA MAKTABA: Maafisa wa kikosi cha umoja wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia (ATMIS)

Serikali ya Somalia inashinikiza kupunguzwa kwa kasi ya kuondoka kwa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Afrika nchini mwake, ikionya kuhusu uwezekano wa ombwe la usalama, kwa mujibu wa nyaraka zinazoonekana na shirika la habari la Reuters.

Hayo yanajiri huku nchi jirani na Somalia, zikiwa na wasiwasi kwamba wanamgambo wa al-Shabaab, wanaweza kunyakua mamlaka.

Kikosi cha Mpito cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), , kinatarajiwa kuondoka ifikapo Desemba 31, huku kikosi kingine kidogo kikitarajiwa kuchukua nafasi yake.

Hata hivyo, katika barua mwezi uliopita kwa kaimu mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, serikali iliomba kuchelewesha kwa mpango huo hadi mwezi Septemba, ambao unanuia kuondolewa kwa nusu ya maafisa 4,000, ambao wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Yaliyomo kwenye barua hiyo, hayakuwa yameripotiwa hapo awali, kwa mujibu wa Reuters.

Serikali hapo awali ilipendekeza, katika tathmini ya pamoja na Umoja wa Ulaya ya mwezi Machi mwaka huu, kwamba ratiba ya jumla ya kuondoka kwa vikosi hivyo irekebishwe "kwa kuzingatia utayari na uwezo" wa vikosi vya Somalia.

Shirika la habari la Reuters liliona pendekezo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG