Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:29

Kenya kupeleka polisi Haiti, kumefuata taratibu zote


Rais wa Kenya Dkt William Ruto, akiwa katika ziara yake ya Kiserekali Washington, DC, Mei 24, 2024.
Rais wa Kenya Dkt William Ruto, akiwa katika ziara yake ya Kiserekali Washington, DC, Mei 24, 2024.

Na Idd Ligongo Hatua ya Kenya, kupeleka polisi wake nchini Haiti kurejesha hali ya utulivu imepitishwa na baraza la mawaziri, mabaraza yote ya bunge, imekidhi vigezo vya kimataifa, na kufuata amri ya mahakama, amesema rais wa Kenya, Dkt William Ruto.

Katika mahojiano maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA), rais Dkt Ruto amesisitiza kwamba kutokana na pingamizi ya mahakama ya Kenya, kuhusu shauri hilo, serikali yake imetekeleza maelekezo ya mahakama yaliyotaka Haiti yenyewe kuingia makubaliano na Kenya.

Dkt Ruto, amesema yeye na Waziri Mkuu wa zamani wa Haiti, Ariel Henry, walishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano hayo jijini Nairobi, ambayo yamefungua njia ikizingatia masharti ya mahakama. Pia aliliomba baraza jipya la utawala la Haiti, kumhakikishia kuyatambua na kuyakubali makubaliano hayo ambapo amehakikishiwa kuwa yamepata baraka zote kwa maandishi.

Amesema kutokana na kufuata taratibu zote za Kenya na Haiti, pamoja na kutambuliwa na utawala wa sasa wa Haiti, atapeleka polisi Haiti kwa kufuata taratibu zote kama Umoja wa Mataifa unavyoelekeza chini ya kanuni za ulinzi wa amani. Kwa maana hiyo amejiridhisha kwamba kupelekwa polisi wa Kenya, nchini Haiti, kumefuata katiba, sheria zote, na kanuni za kimataifa.

Akijibu kwa nini Kenya, imetilia mkazo kupeleka operesheni zake za kusimamia utawala wa sheria Haiti, wakati kuna mizozo mingi Afrika na majirani zake, rais Ruto, amesema Kenya, imehusika katika operesheni za ulinzi wa amani na kusimamia mazungumzo ya kumaliza mizozo katika mataifa jirani. Ilieleka kikosi cha ulinzi wa amani huko Somalia, imeshiriki mchakato wa amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hivi sasa kuna ujumbe wa mapatano ya Sudan Kusini, Nairobi, ili kutatua mzozo huo.

Forum

XS
SM
MD
LG