Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 09:49

Nini mustakabali wa Sheria ya huduma nafuu ya afya "Obamacare" ?


Mgombea urais wa chama cha Demokratik na makamu wa rais Kamala Harris (kulia) na Rais wa Marekani Donald Trump. Picha na AFP
Mgombea urais wa chama cha Demokratik na makamu wa rais Kamala Harris (kulia) na Rais wa Marekani Donald Trump. Picha na AFP

Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya  ACA ambayo pia inajulikana kama “Obamacare,” imeongeza fursa ya huduma za afya kwa mamilioni ya Wamarekani, lakini haiko bayana nini mustakabali wa program chini ya rais ajaye.

Si kampeni ya Harris wala Trump imetoa maelezo kuhusu mtizamo wao kwa sheria hii, lakini wapiga kura wanafuatilia kwa karibu.

Taja Dove ni mmoja wa takriban Wamarekani milioni 25 ambao hawana bima ya afya. Anatafuta mpango ambao utakuwa mbadala kwake hasa kutokana na alivyoona bila ya kuwa na bima.

Taja Dove wa Bima ya Afya ya Lacks anasema: “Huenda nisijisikie vizuri, na nitajaribu kusema, ‘OK’, ndiyo, huenda si jambo kubwa, pengine mafua tu au kitu ambacho si hatari sana. Kwahiyo, naweza kujaribu kulisubirisha kwasababu najua sina bima ya kuilipia lazima niende hospitali.”

Sheria ya Huduma ya Afya ilipitishwa 2010

Sheria ya Huduma ya Afya ilipitishwa mwaka 2010 chini ya utawala wa Obama. Sheria ya mageuzi ya afya inaelezewa kupunguza kwa karibu nusu,

Idadi ya watu ambao si wazee, Wamarekani ambao hawana bima, kwa mujibu wa taasisi sera ya afya – KFF.

Cynthia Cox, wa KFF anaeleza: “Ilileta baadhi ya huduma mpya za bima ya afya katika masoko ambayo hayakuwepo hapo kabla. Na hapa ndipo watu wanaweza kuja kununua bima yao wenyewe na kupatiwa ruzuku ya serikali ili kuifanya iwe ni nafuu zaidi.”

Kuanzia mwezi Machi, Wamarekani milioni 21 walikuwa na biama ya afya kupitia Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya.

Jaribio la Warepublikan Kuifuta Sheria ya "Obamacare"

Warepublican kwa miaka mingi wamejaribu kuifuta sheria hii.

Mshauri wa zamani wa Trump na Rais wa Taasisi ya Paragon Health, Brian Blaise ameorodhesha baadhi ya pingamizi.

Brian Blase, Mshauri wa zamani wa Trump anasema: “ ACA iliweka vikwazo, uimarishaji wa huduma za afya uliongezeka, ambapo mahospitali yalinunua huduma za daktari, watoa huduma za afya waliunganishwa. Na hayo yote yameongeza bei na matumizi na afya ya Mmarekani haijaimarika inavyostahili.”

Wafuasi wa ACA hawakubaliani na hilo. Sasa ni suala kuu katika kampeni ya Harris – Walz katika tiketi ya Democratic.

Mgombea urais Kamala Harris
Mgombea urais Kamala Harris

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic ameeleza: “Ana azma ya kuondoa Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya. Kuturudisha nyuma kwa wakati ambapo makampuni ya bima yalikuwa na mamlaka ya kuwanyima watu ambao walikuwa matatizo ya afya.”

Kama rais, Trump alijaribu na akashindwa kuifuta ACA. Anachukua mwelekeo tofauti katika kampeni yake ya sasa.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Nitaiweka Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya. Si nzuri. Kama tukiwa na kitu kizuri, tutaifanyia kitu. Kama tutafanya vizuri, kwa maana si ya gharama na huduma nzuri ya afya kwako.”

Mgombea urais Donald Trump
Mgombea urais Donald Trump

Si kampeni ya Harris wala ya Trimp imeijibu VOA maombi kutoa maelezo jinsi wagombea wanapanga kuboresha au kuimarisha Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya.

Mshauri wa zamani wa Trump Brian Blasé anaunga mkono kufanyiwa mageuzi badala ya kuifuta ACA.

Brian Blase, Mshauri wa zamani wa Trump anasema: “Kuelekeza sehemu ya ruzuku kutoka kwa bima na kwa watu binafsi.”

Kwa Carl Hughes, na wanaojiandikisha kwenye ACA, hii ni binafsi. Anawasihi watakaoingia White House kutimiza maslahi ya wagonjwa katika mawazo kwa kutathmini mabadiliko.

Carl Hughes, Amejiandikisha Affordable Care Act anasema: “Kuirekebisha itakuwa ni kuiboresha, siyo kuizuia.”

Kando na haki za utoaji mimba na uhamiaji, Hughes, hana chama, anasema ataweka kipaumbele kwa suala la huduma za afya wakati atakapopiga kura yake katika uchaguzi wa Novemba.

Forum

XS
SM
MD
LG