Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 22:02

Peter Mutharika aidhinishwa na upinzani kuwania urais Malawi 2025


Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika (Picha na L. Masina/VOA)
Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika (Picha na L. Masina/VOA)

Mutharika mwenye miaka 84 ambaye alikuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2020 alikubali hatua hii ya upinzani

Chama kikuu cha upinzani nchini Malawi cha Democratic Progress leo Jumapili kimemuidhinisha Rais wa zamani nchini humo Peter Mutharika kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.

Mutharika mwenye miaka 84, ambaye alikuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2020, alisema katika hotuba yake ya kukubali uteuzi, kwamba yeye na chama chake watarekebisha uchumi, ambao ukuaji wake umekuwa si mzuri na umekumbwa na uhaba wa fedha za kigeni ambao umepelekea ukosefu wa mafuta na dawa.

Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika
Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika

Mutharika atakabiliana na Rais Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress, ambaye atakuwa akiwania muhula wa pili katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Septemba 16, 2025. “Tunatokea katika historia ya ushindi kutoka upinzani.

Tutafanya hivyo-hivyo mwaka ujao. Tunakuja kurekebisha uchumi,” Mutharika aliuambia mkutano mkuu wa kitaifa wa chama chake katika mji mkuu wa kibiashara Blantyre.

Forum

XS
SM
MD
LG