Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 12:04

Shambulio dhidi ya mahakama Libya lalaaniwa


Mtu akijiandikisha kupiga kura ndani ya kituo cha kupiga kura Tripoli, Libya Nov. 8, 2021.
Mtu akijiandikisha kupiga kura ndani ya kituo cha kupiga kura Tripoli, Libya Nov. 8, 2021.

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imelaani shambulio dhidi ya mahakama moja katika mji wa kusini wa Sebha kabla ya mwanawe aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi kuwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa tume ya uchaguzi uliokataa ombi lake la kuwania urais.

Serikali ya Libya imewataja wahusika wa tukio hilo la jana Alhamisi lililopelekea mahakama katika mji wa Sebha kufungwa, kuwa ni kundi la wahalifu.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL Ijumaa imelaani pia shambulio hilo na kusema imeshtushwa na tukio hilo na kuonya dhidi ya mashambulio yoyote dhidi ya mchakato kuelekea uchaguzi mkuu wa Libya hapo Disemba 24.

Wakili wa Saif al-Islam Gaddafi, amesema kwamba watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamemzuia kuwasilisha pingamizi yake kupinga kuzuiwa kwa Gaddafi kuwania urais katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Gaddafi anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu - ICC kwa mauaji na ukandamizaji wa raia wakati wa utawala wa baba yake.

Ni miongoni mwa wagombea 25 wa urais ambao maombi yao yalikataliwa, wamepewa saa 48 kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali

XS
SM
MD
LG