Spika wa bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa Libya, Aguila Saleh, leo Jumamosi aliwasilisha nyaraka ili kuwania urais. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Disemba 24 bado kuna mashaka huku kukiwa na mizozo kuhusu kanuni za uchaguzi.
"Nimekuja hapa hivi leo kwenye makao makuu ya tume kuu ya uchaguzi mjini Benghazi, kuwasilisha nyaraka zinazohitajika za kuwania uteuzi kwa nafasi ya rais wa Jamhuri ya Libya, alisema Saleh kwenye televisheni ya “Libya Votes”.