Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:05

Makamu wa Rais Kamala Harris anapanga kuunga mkono Libya kuchukua hatua kuelekea uchaguzi


Makamu rais Kamala Harris akizungumza wakati wa kumbu kumbu ya Martin Luther King, Jr. mjini Washington, Oct. 21, 2021.
Makamu rais Kamala Harris akizungumza wakati wa kumbu kumbu ya Martin Luther King, Jr. mjini Washington, Oct. 21, 2021.

Maafisa waandamizi wa Marekani walitangaza alhamisi kwamba Makamu wa Rais  Kamala Harris anapanga kuunga mkono Libya kuchukua hatua kuelekea uchaguzi katika mkutano wa Paris

Maafisa waandamizi wa Marekani walitangaza alhamisi kwamba Makamu wa Rais Kamala Harris anapanga kuunga mkono Libya kuchukua hatua kuelekea uchaguzi katika mkutano wa Paris wiki ijayo.

Mmoja wa maafisa hao anasema wanataka kuonyesha uungaji mkono wao kwa watu wa Libya wanapoelekea kwenye uchaguzi wa kitaifa na huku wakizingatia umuhimu wa kuondolewa kwa wapiganaji kigeni na mamluki.

Mkutano huo kuhusu Libya, ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, Ujerumani na Italia mjini Paris kuanzia Novemba 12, unatarajiwa kuwakutanisha wakuu wa nchi 20 wa kikanda na kimataifa.

Malumbano kuhusu uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 24 yametishia kuvuruga juhudi za Libya kumaliza muongo mmoja wa machafuko na ghasia. Msukumo mpana wa amani umeweka serikali ya mpito ya umoja madarakani hadi upigaji kura huo.

XS
SM
MD
LG