Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:06

Shakahola kuwa kumbukumbu ya Taifa Kenya


Wafanyikazi wakibeba maiti iliyofukuliwa huko Shakahola na kuipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, terehe 25 Aprili 25, 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Wafanyikazi wakibeba maiti iliyofukuliwa huko Shakahola na kuipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, terehe 25 Aprili 25, 2023. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

Kenya itaubadilisha msitu mkubwa wa Shakahola ulioko pwani ya nchi hiyo kuwa kumbukumbu la kitaifa, eneo hilo ambalo miili ya watu zaidi ya 250 ilifukuliwa na kuhusishwa kuwa ni ya wafuasi wa ibada ya siku ya kiyama, waziri mmoja amesema.

Kiongozi wa dhehebu hilo la kidini Paul Nthenge Mackenzie anakabiliwa na mashtaka mbalimbali katika kesi hiyo kutisha, anayedaiwa kuwaongoza wafuasi wake kwa mahubiria hadi wakafa kwa njaa wakiamini njaa ndiyo njia pekee ya kuelekea kwa Mungu.

Msitu huo "ambao uhalifu mkubwa ulitendeka, hautabaki jinsi ulivyokuwa," Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alisema siku ya Jumanne.

“Serikali itaigeuza kuwa makumbusho ya kitaifa, ni mahali pa kukumbukwa na Wakenya na ulimwengu ambao hauta sahau kilichotokea hapa,” alisema katika taarifa.

Wachunguzi walianza awamu ya tatu ya uchimbaji wa kaburi siku ya Jumanne, na kuibua miili tisa zaidi na kufanya idadi ya vifo kufikia 251.

Kindiki alisema shughuli za ibada ya namna hiyo zilienea nje ya msitu wa Shakahola na hivyo eneo litakalofanyiwa uchunguzi "wa kina, wa kitabibu na wa kisayansi" ulimeongezwa hadi kufikia zaidi ya hekta 14,980.

“Punde zoezi linaloendelea litakapo kamilika, waumini wa dini zote na uongozi wa kitaifa utakutana kwa ajili ya ibada ya ukumbusho,” alisema Kindiki.

Wakati huo huo njaa imeonekana kuwa chanzo kikubwa cha vifo, baadhi ya waathiriwa -- wakiwemo watoto -- walinyongwa, kupigwa au kuzibwa pumzi, kulingana na miili iliyofanyiwa uchunguzi na serikali.

Chanzo cha bahari hii ni Shirika la habari AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG