Wagombea watano wa upinzani walimuariafu Gavana wa Kinshansa katika barua iliyochapishwa siku ya Jumamosi kuhusu azma yao ya kuandaa maandamano.
Lakini matokeo kamili ya uchaguzi bado hayajatangazwa, serikali imesema maandamano yataleta vurugu.
“Maandamano ya kesho yana lengo la kuvuruga mchakato wa uchaguzi-- serikali ya jamhuri haiwezi kukubali hili,” Waziri wa mambo ya nje Peter Kazadi aliwaambia waandishi wa habari. “nawahakikishia kwamba hakutakuwa na maandamano.
Viongozi wa upinzani walio saini barua hiyo ni pamoja na Martin Fayulu – ambaye anadaiwa kushinda katika uchaguzi wa mwisho uliofanyika mwaka 2018 – na Denis Mukwege, mshindi wa tunzo ya Amani ya Nobel, kwa kazi yake ya kuwatibu waathirika wa manyanyaso ya kingono wakati wa vita.
Wameushutumu uchaguzi kuwa “si wa kweli”.
Takribani watu milioni 44, kati ya watu watu millioni 100 wanaoishi katika nchi hiyo kubwa, walistahili kumchagua raisi wao, wabunge wa taifa na mikoa, pamoja na madiwani tika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano.
Kutokana na matatizo mbali mbali ya vifaa vya kupigia kura, upigaji kura uliongezwa muda rasmi kwa siku moja, na maeneo mengine yaliyoko vijijini yaliendelea mpaka siku ya Krismasi. Wapinzani wamedai kulikuwa na “vurugu tupu”
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reueters.
Forum