Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:11

Hofu ya machafuko yakumba mji mkuu wa Haiti


Watu wanaoishi karibu na gereza wakiwa wamebeba mizigo yao waliondoka katika jiji la Port-au-Prince, Haiti, March 4, 2024.Picha na AFP
Watu wanaoishi karibu na gereza wakiwa wamebeba mizigo yao waliondoka katika jiji la Port-au-Prince, Haiti, March 4, 2024.Picha na AFP

Mji mkuu wa Haiti kwa kiasi kikubwa umefungwa, wakaazi wakijitokeza kutafuta mahitaji muhimu huku mamlaka ikiweka hali ya dharura baada ya uvamizi dhidi ya gereza na kusababisha maelfu ya wafungwa kuachiliwa.

Carlotta Pianigiani, mratibu huko Port-au-Prince wa shirika lisilo la kiserikali la matibabu la Alima ameliambia shirika la AFP leo asubuhi shughuli za jiji zilisitishwa na baadhi ya barabara zilifungwa.

Siku ya Jumatatu magenge yenye silaha nzito yalijaribu kutwaa udhibiti wa uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Haiti, yakifyatuliana risasi na polisi na wanajeshi katika shambulio la hivi punde kwenye maeneo muhimu ya serikali katika mlipuko wa ghasia zinazojumuisha kutoroka kwa wafungwa kutoka kwa magereza makubwa mawili ya nchi hiyo.

Viongozi wa magenge kama vile Jimmy Cherisier, anayejulikana kwa jina la utani la Barbecue, wanasema wanajipanga kumwondoa madarakani Waziri Mkuu Henry, ambaye ameongoza taifa hilo lenye matatizo la Caribbean tangu kuuawa kwa rais Jovenel Moise mwaka wa 2021.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alielezea kusikitishwa kwake na "hali ya usalama inayozidi kuzorota" na kutoa wito wa ufadhili zaidi kwa ujumbe uliopangwa wa polisi wa kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG