Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:19

Maelfu ya wafungwa watoroka kutoka gereza la kitaifa Haiti


Gereza ya kitaifa ya Port-au-Prince, Haiti.
Gereza ya kitaifa ya Port-au-Prince, Haiti.

Maelfu ya wafungwa walitoroka Gereza la Taifa la Haiti, lililopo katika mji mkuu, wakati wa makabiliano ya bunduki usiku wa kuamkoa Jumapili, kati ya polisi wa kitaifa na makundi yenye silaha, afisa mmoja aliiambia VOA.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry yuko nje ya nchi kwa sasa. Alienda wiki iliyopita nchini Kenya, ambapo alisaini makubaliano ya pande mbili kuruhusu maafisa 1,000 wa polisi wa Kenya ambao wataongoza kikosi cha usalama cha kimataifa.

Umoja wa Mataifa uliidhinisha kikosi hicho kusaidia Haiti kupambana na vurugu za makundi yenye silaha na kurejesha usalama. Haikuwa wazi alikokuwa waziri huyo mkuu Jumapili.

Afisi ya Rais wa Kenya William Ruto haikujibu ombi la VOA la habari kuhusu mahali alipo Henry. Serikali ya Henry haijatoa taarifa rasmi kuhusu kinachoendelea Haiti. Ubalozi wa Marekani nchini Haiti bado haujatoa maoni yoyote hadharani kuhusu vurugu za mwisho wa wiki.

Waandishi wa habari wa VOA walioenda Jumapili kwenye gereza hilo katikati mwa mji mkuu wa Port-au-Prince na waliona miili ndani na nje ya jengo hilo.

Mhandisi, ambaye hakutaka jina lake litajwa kwa sababu hakuwa amepewa ruhusa ya kuzungumza kwa niaba ya maafisa wa usalama, alisema alikuwa akifanya kazi na polisi wa kitaifa kufanya tathmini ya hali Jumapili asubuhi.

Mhandisi huyo alisema wafungwa 99 walibakia ndani ya gereza. Alisema gereza hilo awali lilikuwa na karibu wafungwa 4,000.

Forum

XS
SM
MD
LG