Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:47

Rwanda kuongoza nchi zinazo zungumza Kifaransa


Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo

Rwanda imepata ushindi wa kidiplomasia kwa kukubaliwa kuongoza jumuiya ya nchi zinazo zungumza Kifaransa (OIF).

Jumuiya hiyo ya kimataifa kwa sauti moja imempitisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kuongoza jumuia hiyo katika mkutano uliofanyika nchini Armenia.

Mushikiwabo, mwenye umri wa miaka 57, amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa umoja huo.

Mushikiwabo ambaye pia aliungwa mkono na Umoja wa Afrika (AU) na Ufaransa, amechaguliwa kiurahisi baada ya mpinzani wake Michaelle Jean raia wa Canada kukosa uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wa Canada.

Rwanda iliamua Kingereza kama lugha muhimu kwenye sekta yake ya elimu na kujiunga na Jumuiya ya Madola (Commonwealth).

Hata hivyo lugha ya Kifaransa imeendelea kuwa lugha rasmi nchini Rwanda.

XS
SM
MD
LG