Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:09

Russia yashambulia usiku kucha mji wa Kherson kwa makombora


Shambulizi la makombora lililofanywa usiku kucha na majeshi ya Russia katika mikoa ya Kherson na Kharkiv.
Shambulizi la makombora lililofanywa usiku kucha na majeshi ya Russia katika mikoa ya Kherson na Kharkiv.

Mashambulizi ya makombora ya usiku kucha katika mji wa kusini mwa Ukraine wa  Kherson yameharibu miundombinu na kuwajeruhi watu watatu , mamlaka za ndani zimesema Jumatatu.

Picha za video zilizotolewa na utawala wa kijeshi wa eneo hilo zimeonyesha matokeo ya mashambulizi makali ya mabomu ya Rusia.

Gavana wa eneo amesema mashambulizi 23 yalifanyika Kherson jumapili.

wizara ya mambo ya ndani nchini Ukraine imeripoti kwamba watu saba akiwemo mtoto wa kike mwenye umri wa siku 23 waliuwawa jumapili.

mapigano katika wiki za karibuni yamefanyika katika maeneo mbalimbali zaidi ya kilomita 1,000 huku Ukraine ikipambana na mashambulizi kwa silaha zinazotolewa na nchi za magharibi na wanajeshi waliofunzwa kutoka nchi za magharibi dhidi ya vikosi vya Russia vilivyovamia ukraine takriban miezi 18 iliyopita.

Wanajeshi wa Ukraine wamepata mafanikio ya ziada tu tangu kuanza kujibu mashambulizi mapema mwezi juni.

Forum

XS
SM
MD
LG