Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:05

Ukraine inasema jeshi la Russia limeua raia saba katika mkoa wa Kherson


Mkazi akipita karibu na nyumba inayoungua iliyoshambuliwa na makombora ya Russia huko Kherson, mkesha wa Krismasi ya Waorthodox, Januari 6, 2023.
Mkazi akipita karibu na nyumba inayoungua iliyoshambuliwa na makombora ya Russia huko Kherson, mkesha wa Krismasi ya Waorthodox, Januari 6, 2023.

Jeshi la Russia lilishambulia kwa makombora mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Kherson Jumapili na kuua raia saba akiwemo mtoto mchanga, maafisa wa Ukraine wamesema.

Wanandoa, mtoto wao wa siku 23 na mwanamme mwingine waliuawa katika kijiji cha Shyroka Balka, waziri wa mambo ya ndani Ihor Klymenko alisema. Mtoto wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka 12 alijeruhiwa vibaya na kufariki akiwa hospitali, aliongeza.

Watu wawili waliuawa na mmoja kujeruhiwa katika kijiji jirani cha Stanislav, ambacho Klymenko alisema kilishambuliwa mara 12 kwa makombora.

Klymenko aliandika kwenye mtandao wa Telegram “ Magaidi hawatasita kamwe kuua raia,” akiweka kwenye mtandao huo picha mbili za nyumba zilizoharibiwa.

Ameongeza kuwa “magaidi lazima wakomeshwe kwa nguvu.”

Watu watatu walijeruhiwa wakati jeshi la Russia lilipoushambulia kwa makombora mji wa Kherson katika shambulio tofauti Jumapili, amesema Andriy Yermak, mkuu wa utawala kwenye ofisi ya Rais wa Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG