Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:21

Russia yarusha makombora Ukraine wakati Zelenskyy yuko Marekani


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika Baraza la Usalama la ngazi ya juu huko New York Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akizungumza katika Baraza la Usalama la ngazi ya juu huko New York Septemba 20, 2023. Picha na ANGELA WEISS / AFP

Mfululizo wa mashambulizi ya makombora yaliyoulenga mji mkuu wa Ukraine, yamewajeruhi watu wasiopungua 45 siku ya Jumatano, wakati rais Volodymyr Zelenskyy akiomba msaada kwa maafisa wa Marekani kuidhinisha msaada mpya wa dola bilioni 61 kuisaidia nchi yake kupambana na uvamizi wa Russia.

Jeshi la anga la Ukraine limesema ulinzi wa anga wa nchi hiyo limeyatungua makombora 10 yaliyorushwa na Russia.

Vifusi vilivyokuwa vinaanguka kutoka kwenye makombora yaliyotunguliwa yameiharibu hospitali ya watoto na mfumo wa maji ya jiji, Meya wa Kyiv, Vitaly Klitschko amesema, wakati Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa jeshi la Kyiv amesema mabaki hayo pia yalidondokea nyumba kadhaa.

Russia imethibitisha kwa mara nyingine tena kwamba ni nchi ya kikatili ambayo imefyatua makombora jana usiku na kuyapiga maeneo ya makazi ya watu, shule za chekechea, na mitambo ya nishati wakati huu wa majira wa baridi” alisema Zelenskyy siku ya Jumatano aliandika kwenye mtandao wa kijamii “Kutakuwa na jibu. Bila shaka.”

Zelenskyy aliongeza kuwa yeye na rais wa Marekani Joe Biden wamekubaliana kuongeza idadi ya mfumo wa ulinzi wa anga, na kuwa Russia “imeonyesha umuhimu wa uamuzi huo”.

Utawala wa Biden siku ya Jumanne ulitangaza msaada mpya wa kijeshi wa mpaka dola milioni 200, msaada ambao unajumuisha ulinzi wa anga wa makombora na vifaa kwa Ukraine kutokana na rasilimali ambazo ziliidhinishwa awali.

Forum

XS
SM
MD
LG