Rais Joe Biden atakuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy huko White House siku ya Jumanne wakati utawala wa Marekani ukiongeza msukumo wake kwa bunge kuidhinisha msaada wa ziada kwa Ukraine katika vita vyake vya kujihami dhidi ya Russia.
Ziara hiyo inalenga kusisitiza dhamira ya Marekani isiyotetereka ya kuwasaidia watu wa Ukraine wakati wakijitetea dhidi ya uvamizi wa kikatili wa Russia, White House imesema katika taarifa yake Jumapili.
Ofisi ya Zelenskyy ilithibitisha kuwa amekubali mwaliko wa Biden. Pia amealikwa kuzungumza kwenye mkutano wa maseneta wote.
Biden anawaomba wabunge katika Bunge kutoa dola bilioni 110 za mfuko wa fedha wa vita kwa Ukraine (dola bilioni 61.4) na Israel, pamoja na vipaumbele vingine vya usalama wa taifa. Lakini siku ya Jumatano, Wa-Republican katika bunge la seneti la Marekani walizuia mswaada huo, wakisema mabadiliko makubwa ya usalama wa mpaka wa Marekani yalihitajika.
Forum