Jeshi la anga la Ukraine limesema mifumo yake ya anga ilitungua makombora yote ya masafa marefu yaliyorushwa na Russia.
Mabaki ya makombora yaliyorushwa na ndege zisizokuwa na rubani yaliharibu hospitali moja ya watoto na mfumo wa maji, meya wa mji wa Kyiv Vitaly Klitschko amesema.
Zelenskiy alisema leo kwenye mitandao ya kijamii “ Russia imethibitisha kwa mara nyingine kuwa ni nchi yenye ukatili kwa kurusha makombora usiku, ikijaribu kushambulia maeneo ya makazi, shule za chekechea na miundombinu ya nishati wakati wa msimu wa baridi.”
Utawala wa Biden Jumanne ulitangaza msaada mpya wa kijeshi wa hadi dola milioni 200 kwa Ukraine.
Forum