Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:07

Russia yamfunga gerezani mwandishi wa radio inayofadhiliwa na Marekani


Mhariri wa Radio RFE/RL inayofadhiliwa na serikali ya Marekani, Alsu Kurmasheva, akiwa mahakamani wakati kesi yake ikisikilizwa Mei 31, 2024 Picha na AP.
Mhariri wa Radio RFE/RL inayofadhiliwa na serikali ya Marekani, Alsu Kurmasheva, akiwa mahakamani wakati kesi yake ikisikilizwa Mei 31, 2024 Picha na AP.

Mahakama moja ya Russia imemtia hatiani Alsu Kurmasheva, mwandishi wa habari mwenye asili ya Russia aliyekuwa akifanya kazi kwenye Radio Free Europe/Radio Liberty inyofadhiliwa na serikali ya Marekani.

Mwandishi huyo wa habari alituhumiwa kwa kusambaza habari za uongo kuhusu jeshi ya Russia na kuhukumiwa miaka sita na nusu gerezani kufuatia kesi hiyo ya siri, rekodi za mahakama na maafisa walisema Jumatatu.

Hukumu hiyo ilitolewa huko Kazan, mji mkuu wa mkoa wa Tatarstan wa Russia ulioko katikati, alikuja siku ya Ijumaa, siku hiyo ambayo mahakama ya jiji la Yekaterinburg huko Russia ilimtia hatiani mwandishi wa Wall Street Journal Evan Gershkovich kwa tuhuma za ujasusi na kumuhukumu miaka 16 jela, kesi ambayo Marekani inaiita kuwa ni ya kisiasa.

Kurmasheva, mwenye umri wa miaka 47- mhariri wa RFE/RL, idhaa ya lugha ya Tatar-Bashkir, amehukumiwa kwa “kusambaza habari za uongo” kuhusu jeshi, kulingana na tovuti ya mahakama kuu ya Tatarstan. Msemaji wa mahakama Natalya Loseva alidhibitisha hukumu ya Kurmasheva na kuifichua hukumu hiyo kwa shirika la habari la Associated Press kwa njia ya simu katika kesi hiyo inayoainishwa kuwa ya siri.

Alisema mwaka jana mashitaka hayo yalitokana na kitabu cha Idhaa ya Tatar-Bashkir kilichotolewa mwaka 2022 kikiitwa “Hapana Vita” —“ mkusanyiko wa hadithi fupi za Warussia ambao hawataki nchi yao kuwa vitani na Ukraine.”

Alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa RFE/RL Stephen Capus aliishitumu kesi hiyo na kuhukumiwa kwa Kurmasheva kuwa kama “dhihaka ya haki.”

Forum

XS
SM
MD
LG