Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 22:39

Rishi Sunak akutana na El-Sisi mjini Cairo


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi mjini Cairo kuonyesha msimamo wa nchi yake katika kushughulikia mzozo wa Israel na Palestina.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi mjini Cairo kuonyesha msimamo wa nchi yake katika kushughulikia mzozo wa Israel na Palestina.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alikutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi mjini Cairo Ijumaa kuonyesha msimamo nchi yake katika kushughulikia mzozo wa Israel na Palestina.

Kwenye ziara yake ya Mashariki ya Kati Sunak alielezea kuguswa na vifo vya raia kufuatia mashambulizi kati ya Israel na Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa mjini Cairo.

Akizungumza na marais wa Misri na Palestina kwa nyakati tofauti, Sunak alitoa pole kwa rais Mahmoud Abbas ambapo kwa sasa yupo Misri akitazamiwa kuwa mmoja wa watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa amani uliopangwa kufanyika Jumamosi kufuatia kadhia inayoendelea katika ardhi ya Palestina.

Akizungumza na mwenyeji wake Rais Abdel Fattah El-Sisi, Sunak alipongeza "juhudi chanya za Misri pia katika mzozo unaoendelea."

Rishi Sunak apokelewa na mwenyeji wake Abdel Fattah Ekl-Sisi mjini Cairo
Rishi Sunak apokelewa na mwenyeji wake Abdel Fattah Ekl-Sisi mjini Cairo

Aidha alihimiza kuendeleza mawasiliano zaidi ndani ya kipindi hiki cha mzozo.

Waziri Mkuu Sunak aliweka wazi kuwa Uingereza inaamini umuhimu wa kutuma misaada kwa watu wa Palestina na kuifikisha kupitia Misri.

Imetayarishhwa na Shafii Mbinda, Sauti ya Amerika, Cairo, Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG