Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 15:58

Ramaphosa kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri Jumatatu


Raia wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Raia wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa atatangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu, msemaji wa rais, Vincent Magwenya, alisema Jumapili.

Mabadiliko ya baraza la mawaziri yamekuwa yakitarajiwa kwa kiasi kikubwa tangu Ramaphosa kuchaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC) kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa chama mwezi Disemba mwaka jana, na kumfungulia njia ya kuwania muhula wa pili mwaka 2024.

“Rais anakamilisha uundaji upya wa Halmashauri Kuu ya Taifa,” Magwenya alisema kwenye kikao na waandishi wa habari na kuongeza kuwa rais huyo alikuwa anasubiri kuapishwa kwa baadhi ya wabunge kabla ya kutangaza mabadiliko hayo.

Ramaphosa anatarajiwa kumteua naibu rais mpya baada ya afisi ya rais kutangaza kujiuzulu kwa David Mabuza kutoka wadhifa huo siku ya Jumatano. Nafasi mpya ya waziri wa umeme ni miongoni mwa zile zitakazojazwa.

Rais huyo alitangaza mwezi uliopita kwamba angebuni nafasi ya waziri wa umeme ili kusaidia kutatua mzozo wa kitaifa wa umeme, huku kampuni ya Eskom ikiendelea na mgao wa umeme wenye utata zaidi katika historia.

XS
SM
MD
LG