Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 22:45
VOA Direct Packages

Museveni akutana na Ramaphosa kwenye ziara ya Afrika Kusini


Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha ya maktaba
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha ya maktaba

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameomba kuimarishwa zaidi kwa ushirikiano wa kibiashara miongoni mwa mataifa ya kiafrika huku akilalamikia gharama ya juu ya kununua bidhaa pamoja na huduma kutoka nje ya bara hilo.

Hayo ameyasema Jumanne wakati akianza ziara rasmi Afrika Kusini, kwa nia ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Uganda na taifa hilo lililoendelea zaidi barani Afrika. Rais Yoweri Museveni alikutana na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, akiwa pamoja na baadhi ya mawaziri wake wakitarajiwa kutia saini mikataba kadhaa ya kibiashara na wenzao wa taifa hilo.

Akizungumza kabla ya kukutana na Ramaphosa, Museveni alisisitiza umuhimu wa biashara kati ya mataifa ndani ya bara, wakati pia akiangazia baadhi ya changamoto zinazozuia hilo kufanyika. Museveni amesema kwamba ni muhimu kwa bara hilo kuwa na amani ili kuweka mazingira mema ya kibiashara kati ya mataifa.

Ramaphosa kwa upande wake alisema kwamba anaitazama Uganda kama mshirika wa karibu kutoka Afrika Mashariki, na kupongeza mchango wake katika kukuza uchumi wa kieneo, ushirikiano wa kisiasa pamoja na amani na uthabiti wa kieneo. Amesema kwamba taifa lake lina wasi wasi kuhusu hali ilivyo huko Jamahuri ya kidemokrasia ya Congo. Amesema kwamba wanakemea vikali ghasia zinazofanywa na makundi yenye silaha.

Kati ya 2017 na 2021 jumla ya thamani ya kibiashara kati ya mataifa yote mawili ilifikia dola milioni 162 za kimarekani.

Upelekaji wa bidhaa nchini Uganda kutoka Afrika Kusini mwaka 2018 ulikuwa wenye thamani ya dola 169 za kimarekani, wakati bidhaa kutoka Uganda kuingia Afrika Kusini zikiwa na thamani ya dola milioni 6.8 mwaka 2017 na dola milioni 17.5 kufikia 2020.

XS
SM
MD
LG