Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:15

Rais Ruto akutana na Mkurugenzi wa CIA


William Burns
William Burns

Rais wa Kenya Dr. William Ruto amekutana na mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA William Burns katika kikao ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa ujasusi wa Kenya Noordin Haji.

Noordin Haji
Noordin Haji

Ruto ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kikao hicho kwamba amani na usalama katika eneo hilo umeimarika kwa kiwango kikubwa kutokana na ushirikiano kati ya Kenya na washirika wake kote duniani.

William Ruto
William Ruto

Ruto amesema kwamba uongozi wa eneo hilo utaendelea kuwa imara dhidi ya uhalifu na kulinda amani na utulivu, demokrasia na ukuaji wa uchumi.

Yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo hayajawekwa wazi.

Hii ni mara ya pili mkurugenzi mkuu wa idara ya ujasusi ya Marekani anaitemebelea Kenya mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG