Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:12

Rais Mteule wa Senegal aapishwa


Bassirou Diomaye Faye (kushoto) akiapishwa kuwa rais wa Senegal huko Diamniadio karibu na mji mkuu wa Dakar on Aprili 2, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP
Bassirou Diomaye Faye (kushoto) akiapishwa kuwa rais wa Senegal huko Diamniadio karibu na mji mkuu wa Dakar on Aprili 2, 2024. Picha na JOHN WESSELS / AFP

Bassiroe Diomaye Faye mwanasiasa wa mrengo wa kushoto, mtetezi wa Umoja wa Afrika ameapishwa Jumanne kama rais mwenye umri mdogo zaidi wa Senegal baada ya kupata ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Rais huyo mpya ametoa ahadi ya kuleta mabadiliko makubwa siku 10 tu baada ya kuachiliwa huru kutoka jela.

Rais Faye mwenye umri wa miaka 44 hajawahi kuongoza ofisi yoyote kabla ya kuchaguliwa lakini viongozi mbalimbali wa Afrika wameudhuria sherehe hizo katika mji mpya wa Diamniadio karibu na mji wa Dakar.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliohudhuria ni rais wa mpito wa Guinea Mamady Doumbouya na raia wa Nigeria Bola Ahmed Tunubu.

Faye Ameapa kuzingatia kwa uangalifu kanuni za katiba na sheria na kutetea uadilifu katika nchi nzima na uhuru wa taifa na kutoacha nyuma juhudi zozote za kufikia umoja wa Afrika.

“Kwa kiwango cha Afrika changamoto za usalama, zinatulazimisha tuwe na umoja zaidi,” amesema hayo mbele ya mamia ya maafisa na viongozi kadhaa wa afrika kwenye ukumbi wa maonyesho wa Diamniadio.

“Barani afrika, kiwango cha changamoto za usalama zinazotukabili na changamoto nyenginezo nyingi ambazo tunabidi kuzitanzua zitatulazimu kuonesha umoja zaidi kati yetu. Ninaweza kusikia sauti ya wasomi wetyu wakipaza sauti zao kuhusu dhamira zetu za pamoja za kuwa na uhuru zaidi, maendeleo na ustawi wetu” alisema rais huyo mpya wa Senegal.

Faye amekabidhiwa rasmi madaraka na rais aneyondoka madarakani Macky Sall katika ikulu Dakar baada ya sherehe za kula kiapu kufanyika katika mji mpya wa Diamniadio.

Faye, Mkaguzi wa kodi wa zamani amekuwa rais wa tano wa Senegal tangu kupata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka 1960 na amekiri hadharani kuwa na wake wawili.

Forum

XS
SM
MD
LG