Mshambualiaji baadaye alijiua mwenyewe. Msemaji wa polisi anasema watu kadhaa wengine walijeruhiwa jana Alhamisi usiku katika tukio hilo.
Watu wanne wamelazwa hospitali, akiwemo mtu ambaye ana majeraha mabaya.
Mtu mwingine wa pili alitibiwa kwenye eneo la tukio. Mfyatuaji risasi bado hajatambuliwa.
Polisi bado wako katika eneo la tukio kuhoji watu nyakati za alfajiri hivi leo Ijumaa.
Eneo hilo la tukio liko karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege wa Indianapolis.