Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:50

Paul Rusesabagina kuachiwa huru


Paul Rusesabagina (katikati) akiwasili katika mahakama ya haki iliyoko Nyarugenge mjini Kigali, Rwanda. Picha na Simon Wohlfahrt / AFP.
Paul Rusesabagina (katikati) akiwasili katika mahakama ya haki iliyoko Nyarugenge mjini Kigali, Rwanda. Picha na Simon Wohlfahrt / AFP.

Serikali ya Rwanda itawaachilia huru kiongozi wa kundi la upinzani la Rwanda Movement for Democratic Change (MRCD) Paul Rusesabagina na msemaji wa kundi la Forces for National Liberation (FLN) Callixte Nsabimana waliokuwa wakitumikia kifungo kwa tuhuma za ugaidi.

Watuhumiwa hao wataachiwa huru siku ya Jumamosi, kufuatia amri kutoka kwa rais Paul Kagame, kulingana na taarifa kutoka wizara ya sheria na ofisi ya mwanasheia mkuu wa Rwanda.

Rusesabagina, mkosoaji mkubwa wa Kagame, alikiri kuwa na nafasi ya uongozi katika kundi la upinzani, Rwanda Movement for Democratic Change (MRCD), lakini alikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Rwanda na wafuasi wake wenye silaha wa kundi la Forces for National Liberation (FLN).

Paul Rusesabagina, ambaye alionyeshwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood "Hotel Rwanda"alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 25 jela nchini Rwanda.

Kuachiliwa kwake kunafuatia msukumo mkali wa kidiplomasia ulioanywa na Marekani ambako Rusesabagina ana haki ya ukaazi wa kudumu.

Rais mstaafu wa Marekani George W. Bush akimtunikia tunzo ya Urais ya nishani ya uhuru. Picha na Mandel NGAN/AFP.
Rais mstaafu wa Marekani George W. Bush akimtunikia tunzo ya Urais ya nishani ya uhuru. Picha na Mandel NGAN/AFP.

Kihistoria uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili umeingia dosari baada ya kesi hiyo, pamoja madai kuwa Rwanda inahusika katika mgogoro unaoendelea huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rusesabagina alihukumiwa mwezi Septemba mwaka 2021 kutokana na uhusiano wake na taasisi inayopinga utawala wa Kagame. Rusesabagina alikanusha mashtaka yote na pia alikataa kushiriki katika kesi hiyo ambayo yeye na wafuasi wake waliiita kuwa ni udanganyifu wa kisiasa.

Rusesabagina kwanza atasafirishwa kwa ndege kwenda Doha, nchini Qatar, na baadaye kuelekea Marekani, chanzo cha habari kilisema.

Washington inamuona Rusesabagina kama mtu "aliyeshikiliwa kimakosa", sababu moja wapo ni kutokana na kile ilichokiita ukosefu wa dhamana haki katika kesi hiyo.

Kuachiliwa kwa aliyekuwa mmiliki wa hoteli Rwanda huenda kukapunguza mivutano na Marekani, ambayo imekuwa ikirejea kuitaka Rwanda kutoliunga mkono kundi la waasi la M23 na kuyaondoa majeshi yake katika nchi jirani ya Kongo. Hata hivyo Rwanda imekanusha kuhusika katika mgogoro wa Kongo.

"Najuta kutochukua tahadhari zaidi kuhakikisha kuwa wanachama wa muungano wa MRCD wanazingatia kikamilifu kanuni za kutotumia ghasia," Rusesabagina aliandika katika barua ambayo Sauti ya Ameirika imeiona ya Oktoba 14 kwa Kagame akitaka amhurumie.

"Iwapo nitapewa msamaha na kuachiliwa huru, naelewa fika nitatumia siku zangu zilizosalia nchini Marekani nikitafakari kwa utulivu," aliandika.

Msemaji wa FLN Callixte Nsabimana, anayejulikana kwa jina la Sankara, ambaye alitiwa hatiani na mahakama ncinini Rwanda kwa tuhuma za ugaidi, mauaji na utekaji nyara mwaka 2019, Naye pia ataachiliwa huru akiwa pamoja na Rusesabagina na watu wengine watatu, Taarifa ya wizara ya sheria na ofisi ya mwanasheria mkuu imesema.

Mapema mwezi huu, Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kulikuwa na mijadala kuhusu "kusuluhisha" hatima ya Paul Rusesabagina.

XS
SM
MD
LG