Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:50

Zaidi ya watu 100,000 wapoteza makazi DRC kutokana na mashambulizi


Jeshi la DRC likifika katika tukio la mlipuko wa bomu.
Jeshi la DRC likifika katika tukio la mlipuko wa bomu.

Huko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo duru zinaeleza kwamba mfululizo wa mashambulizi dhidi ya raia huko Kivu Kaskazini yamesabaisha kupoteza makazi kwa zaidi ya watu 100,000 na kusababisha kupotea kwa darzeni  ya maisha katika wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa walizopata Umoja wa Mataifa wa kibinadamu kutoka kwa washirika wa kibinadamu zaidi ya watu 50,000 wamekoseshwa makazi kutoka Rutshuru nakutafuta sehemu salama huko Kibirizi wakati baadhi ya watu 55,000 kutoka Masisi walikimbilia vijiji jirani pamoja na Goma na kuelekea Minova huko Kivu Kusini.

“Wenzetu wa kulinda amani nchini humo wanaripoti kwamba waliwahifadhi watoto 95 katika kambi yao ya Sake; hiyo ni pamoja na watoto 50 kutoka kituo cha watoto yatima. Hii ilitokea kufuatia mapigano ya wikendi katika eneo hili kati ya vikosi vya ulinzi vya Kongo na kundi la waasi la M23" alisema Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric.

“Raia wanne walifariki wakati wa mapigano hayo na takriban wengine watano kujeruhiwa. Wanajeshi wa kulinda amani walitoa msaada wa kimatibabu kwa waliojeruhiwa kwenye kituo chao na baadaye kuwahamisha hadi Goma. Watoto hao pia walihamishiwa katika kituo cha watoto huko Goma” aliongeza Dujjarric.

Ujumbe huo wa MONUSCO pia uliripoti kwamba tangu mwanzoni mwa mwezi Machi kundi la waasi la ADF (Allied Democratic Forces) limeripotiwa kuwaua takriban raia 97 katika eneo la Beni katika Mkoa wa Kivu Kaskazini. Kama walivyotaja wiki iliyopita, kutokana na operesheni za pamoja zinazoendelea kati ya vikosi vya ulinzi vya Uganda na Congo walinda amani wa Umoja wa Mataifa hawawezi kufika eneo la kusini mwa Beni ambako watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa ADF walifanya mashambulizi haya.

XS
SM
MD
LG