Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:44

Papa Francis kuzuru Sudan Kusini Julai


Papa Francis (Vatican Media/­Handout via REUTERS)
Papa Francis (Vatican Media/­Handout via REUTERS)

Uongozi wa Vatican umesema Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis atafanya ziara hiyo ambayo imecheleweshwa mara kadhaa kutokana na sababu za kiusalama.

Hii inatokana na kuwepo kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya nchi hiyo kupata uhuru.

Mwezi Julai utakuwa ni maadhimisho ya miaka 11 tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka kwa Sudan.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalianza mwaka 2013, miaka miwili baada ya uhuru huo, na kusababisha vifo vya watu 400,000.

Pande kuu zinazo zozana zilisaini mkataba wa amani mwaka 2018 lakini njaa na mapigano yanatokea kila mara kote nchini humo.

Viogozi wa Vatican wamesema kwamba Papa Francis atakuwa Juba, Sudan kusini kuanzia July 5 hadi 7 baada ya kutembelea miji ya Kinshasa na Goma, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

XS
SM
MD
LG