Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:51

Papa Francis apongeza mchango wa wanawake katika salamu za mwaka 2022


Papa Francis akiwa Vatica, Dec. 31, 2021. REUTERS/Remo Casilli
Papa Francis akiwa Vatica, Dec. 31, 2021. REUTERS/Remo Casilli

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis katika salamu zake za mwaka mpya Jumamosi amepongeza ujuzi wa wanawake katika kuhamasisha amani duniani, na kuilinganisha ukatili dhidi ya wanawake kuwa ni dhambi dhidi ya mwenyenzi mungu.

Kanisa Katoliki linaadhimisha Januari 1 kuwa siku iliyotengwa kwa ajili ya amani ya duniani, na ibada aliyoiendesha asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Peter mjini Vatican ilipongeza nafasi maalum katika imani kama mama wa Yesu.

“Kinamama “wanafahamu namna ya kukabiliana na vikwazo na kutokukubaliana, na kuleta amani,” Francis alisema wakati wa ibada hiyo.

“Katika njia hii, wanageuza matatizo kuwa fursa kwa ajili ya kurejesha kuzaliwa upya na ukuaji. Wanaweza kufanya hivi kwa sababu wanajua namna ya “kuendeleza” mshikamano katika nyanja mbalimbali za maisha,” Papa alisema. “Tunawahitaji watu kama hawa, wenye uwezo kufuma nyuzi za umoja zilizokuwepo kuondokana na nyaya zenye kuchoma za migogoro na migawanyiko.”

Francis amemsihi kila mtu kufanya juhudi kuwaendeleza kina mama na kuwalinda wanawake.

“Ni kiasi gani cha uhalifu kinaelekezwa dhidi ya wanawake! Inatosha! Kumdhuru mwanamke ni kumkosea Mungu, ambaye kupitia mwanamke ameuumba wanaadamu,” papa alisema, akiizungumzia imani ya Kikristo kuwa Yesu alikuwa mtoto wa Mungu.

Alielekeza pongezi nyingi kwa wanawake, ikiwemo kina mama, akisema wao “wanauangalia ulimwengu siyo kwa ajili ya kuunyonya lakini kuwezesha kuwepo maisha. Wanawake ambao, wanaona kwa nyoyo zao, wanaweza kuunganisha ndoto na matakwa yao kwa kuyafikia kiuhakika, bila ya kuanguka katika vizuizi na maendeleo yenye kufeli.

Wakati akiahidi katika uongozi wake kuwapa wanawake majukumu makubwa zaidi katika kanisa, Francis pia ameweka wazi kuwa upadri ni kwa wanaume tu.

Katika ujumbe wake wa Twitter kabla ya Ibada ya Siku Mwaka Mpya, Francis alifafanua matumaini yake na mikakati kwa ajili ya amani.

“Wote tunaweza kushirikiana kuijenga dunia yenye amani zaidi, ikianzia kutoka katika moyo wa kila mtu na mahusiano katika familia, halafu katika jamii na mazingira yetu, na kuendelea kupanda juu kufikia mahusiano kati ya watu na mataifa,” Francis alituma alitweet.

Ukimtoa papa na wana kwaya kundi lilioundwa na wavulana na watu wazima, washiriki wote waliokuwepo katika ibada hiyo walivaa barakoa ikiwa ni tahadhari dhidi ya COVID-19.

Francis, ambaye ana umri wa miaka 85 na aliyechanjwa dhidi ya virusi vya corona, alivaa barakoa inayotumika katika upasuaji wakati wa ibada ya Mwaka Mpya ambayo iliendeshwa na kadinali wa Vatican. Ilikuwa ni tukio nadra la kuepuka kuvaa barakoa katika sherehe za umma katika kipindi cha miaka miwili ya janga hilo.

Chanzo cha Habari Hii ni Shirika la Habari la AP

XS
SM
MD
LG