Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:13

Kanisa Katoliki la Uhispania litaanzisha uchunguzi kuhusu madai ya manyanyaso ya kingono

Papa Francis akisalimiana na waandishi wa habari kwenye ndege ya Papa wakati wa ziara yake ya kichungaji huko Cyprus na Ugiriki, Desemba 6, 2021.(Alessandro Di Meo/Pool photo via AP)
Papa Francis akisalimiana na waandishi wa habari kwenye ndege ya Papa wakati wa ziara yake ya kichungaji huko Cyprus na Ugiriki, Desemba 6, 2021.(Alessandro Di Meo/Pool photo via AP)

Kanisa Katoliki la Uhispania litaanzisha uchunguzi kuhusu madai ya unyanyasaji wa kingono kwa mamia ya watoto na makasisi ikiangazia kuanzia  miaka 80 iliyopita ambayo gazeti la El Pais limefichua, gazeti hilo  la kila siku lilisema Jumapili.

Uchunguzi huo utafuatilia madai ya unyanyasaji dhidi ya makasisi 251 na baadhi ya waumini kutoka taasisi za kidini ambazo gazeti hilo limefichua, El Pais alisema.

Gazeti hilo halijachapisha kwa ukamilifu matokeo yake kutokana na uchunguzi wa miaka mitatu ilioufanya kuhusiana na suala hilo, lakini lilisema mwandishi wake alikabidhi ripoti yake ya kurasa 385 kwa Papa Francis Desemba 2 wakati msafara wa papa na waandishi wa habari walipokuwa wakisafiri kwa ndege kutoka Roma kwenda Cyprus.

Idadi ya waathirika ni takriban 1,237 lakini inaweza kuongezeka hadi maelfu, gazeti hilo lilisema. Madai hayo yanahusu mashirika 31 ya kanisa katoliki na Dayosisi 31 kati ya 70 za nchi hiyo. Kesi ya zamani zaidi ni ya mwaka 1942 na ya hivi karibuni zaidi ni mwaka 2018.

Uchunguzi huo utafanywa na kongamano la maaskofu wa Uhispania, ambalo linaongozwa na Kardinali Juan Jose Omella, askofu mkuu wa Barcelona, kulingana na El Pais.

XS
SM
MD
LG