Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:47

Pande hasimu zaendelea na mapigano Sudan, wakaazi wa Khartoum mashakani


Gari za kijeshi zilizoteketezwa zikiwa katika upande wa kusini wa Khartoum, Sudan, Aprili 20, 2023. Picha na AP / Marwan Ally
Gari za kijeshi zilizoteketezwa zikiwa katika upande wa kusini wa Khartoum, Sudan, Aprili 20, 2023. Picha na AP / Marwan Ally

Milipuko na milio ya risasi imeendelea kusikika katika mji mkuu wa Sudan Alhamisi wakati mapigano baina ya vikosi vya wanajeshi wawili mahasimu vikionyesha hakuna ishara ya kupungua mapigano  kabla ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Karibu watu 300 waliuwawa tangu mapigano kuzuka Jumamosi baina ya vikosi vitiifu kwa mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fatah al- Burhan na msaidizi wake Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza kikosi vya wanamgambo cha RSF.

Baadhi ya mapigano makali yametokea katika mji mkuu wa Khartoum wenye watu milioni tano wengi wao wakiwa wamekwama katika nyumba zao bila umeme, chakula, na maji.

Mapigano hayo yanaingia siku ya sita baada ya sitisho jingine la mapigano kushindwa kufanya kazi na milio ya risasi ikiendelea kusikika na moshi mweusi ukitanda kwenye majengo kuzunguka Khartoum, uwanja wa ndege wa kimataifa na makao makuu ya jeshi kwenye mji mkuu.

The RSF ilisema vikosi vyake vitaweka nia ya dhati ya kusitisha mapigano kabisa kama ilivyofanya jeshi kuanzia jana kwa saa 24, lakini mashahidi wanasema mashambulizi ya risasi hayakusimama katika mji mkuu wa Khartoum kuanzia muda uliopangwa na hadi usiku, kwa sababu usitishwaji mwingine wa mapigano ulikiukwa ndani ya dakika chache kabla ya kuanza .

XS
SM
MD
LG