Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:18

Maelfu ya wakazi wa Khartoum waukimbia mji


Wakazi wa mji wa Khartoum wakivikimbia vitongoji vyao huku mapigano yakiendelea tarehe 19 Aprili, baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya saa 24. Picha na shirika la habari la AFP
Wakazi wa mji wa Khartoum wakivikimbia vitongoji vyao huku mapigano yakiendelea tarehe 19 Aprili, baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya saa 24. Picha na shirika la habari la AFP

Maelfu ya wakazi wa mji mkuu wa Sudan wameukimbia mji huo siku ya Jumatano, wakati mashahuda walisema maiti zilionekana zimesambaa mitaani kutokana na mapigano kati ya jeshi na vikosi vya RSF.

Mapigano ya siku tano mjini Khartoum na kwingineko katika nchi hiyo iliyoko kaskazini mashariki mwa Afrika yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 270, balozi za kigeni zilisema Jumatano.

Wanadiplomasia wa kigeni walishambuliwa, mratibu Umoja wa Mataifa anayeshughulikia misaada ya dharura, Martin Griffiths alisema Umoja wa Mataifa ulipokea "ripoti za mashambulizi na manyanyaso ya ngono dhidi ya wafanyakazi wa misaada".

Serikali imeanza kupanga mipango ya kuwahamisha raia wao, miongoni mwao wafanyakazi wengi wa Umoja wa Mataifa.

Ghasia hizo zilizuka siku ya Jumamosi kati ya vikosi vya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya 2021: mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza vikosi vya Rapid Support Forces (RSF).

Mapigano hayo yanafuatia mzozo mkali kati yao kuhusu mpango wa ujumuishaji wa vikosi vya RSF katika jeshi la kawaida -- sharti muhimu katika makubaliano ya mwisho yenye lengo la kurejesha mpito wa kidemkorasia nchini Sudan.

"Maisha mjini Khartoum yatakuwa mabaya kama vita hivi havitasitishwa," alisema Alawya al-Tayeb, mwenye umri wa miaka 33, wakati akiutoroka mji huo mkuu.

"Nilijitahidi kuwaficha watoto wasione maiti za watu waliouawa zilizozagaa mitaani," alisema, na akiongeza kuwa watoto wake kwa sasa wanakabiliwa natatizo la mshtuko na watahitaji matibabu.

Chanzo cha nabari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG