Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:46

Sudan yatangaza sitisho la mapigano kwa saa 24 tu.


SUDAN-POLITICS-UNREST
SUDAN-POLITICS-UNREST

Makamanda wapinzani wa Sudan walikubaliana kusitisha mapigano kwa saa 24 kuanzia Jumanne jioni, baada ya shinikizo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuhusu mapigano makali yaliyokumba mji mkuu Khartoum, pamoja na kushambuliwa kwa msafara wa wanadiplomasia wa Marekani.

Mgogoro kati ya makundi tawala nchini Sudan ulizuka siku nne zilizopita na umesababisha vifo vya takriban watu 185 nchini kote, na kusababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa umekitaja kuwa janga kubwa la kibinadamu, ikiwa ni pamoja na hatari ya kuporomoka kwa mfumo wa afya.

Jenerali wa Jeshi Shams El Din Kabbashi, mjumbe wa baraza tawala la kijeshi la Sudan, alisema kwenye televisheni ya al Arabiya kwamba usitishaji mapoigano utaanza kutekelezwa saa kumi na mbili jioni saa za Sudan, lakini kwa kipindi cha saa 24 tu.

Mapema leo, milio ya risasi ilisikika kote Khartoum ikiambatana na milio ya ndege za kivita na milipuko. Wakazi katika miji jirani ya Omdurman na Bahri waliripoti mashambulio ya anga ambayo yalitikisa majengo. Mapigano pia yamepamba moto magharibi mwa nchi, Umoja wa Mataifa ulisema.

Blinken alizungumza kwa njia ya simu, kwa nyakati tofauti, na makamanda wawili wanaozozana.

Awali Blinken alilaani shambulizi lililolenga msafara wa maafisa wa kidiplomasia wa Marekani akisema ulishambuliwa licha ya magari hayo kuwa na namba za leseni za kidiplomasia na kuwa na bendera za Marekani.

XS
SM
MD
LG