Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:16

Jaribio jipya la kusitisha mapigano lagonga mwamba Sudan


Mwanamume akikagua magari yaliyoharibiwa nje ya makao makuu ya vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum mnamo Aprili 19, 2023. Picha na AFP.
Mwanamume akikagua magari yaliyoharibiwa nje ya makao makuu ya vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) huko Khartoum mnamo Aprili 19, 2023. Picha na AFP.

Jaribio jipya la kusitisha mapigano lilishindikana Jumatano, na kuwaacha watu wakiwa na hofu kuhusu kupungukiwa na chakula wakati wengi wao wakiwa wamekwama majumbani mwao.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 24 yalipaswa kuanza kutekelezwa saa kumi na mbili jioni, lakini mashahidi wawili waliliambia shirika la habari la Reuters kuwa walishuhudia mapigano yakiendelea katika maeneo tofauti ya mji mkuu wa Sudan.

Tangazo la Jumatano la kusitisha mapigano lilikuwa linafuatia makubaliano ya awali ya yaliyofanywa Jumanne na kusimamiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na viongozi wengine wa kimataifa lakini walikabiliwa na upinzani kutoka kwa pande hasimu ambazo ziliendelea kupigana.

Siku ya Jumatano ujumbe wa kidiplomasia nchini Sudan ulitoa wito kwa vikosi vya jeshi vinavyo shambuliana kusitisha mapigano na kuzingatia wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kuwalinda raia, wanadiplomasia na wahusika wa masuala ya kibinadamu kufuatia mzozo mkubwa wa siku nyingi wa kugombea madaraka katika maeneo mbalimbali nchini himo.

Ujumbe huo uliwajumuisha mabalozi wa nchi za Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uholanzi, Norway, Poland, Jamhuri ya Korea, Uhispania, Uswizi, Sweden, Uingereza, Marekani, na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya.

Katika taarifa ya pamoja, walilisihi jeshi na kikundi chenye nguvu cha kijeshi kuepusha kuongezeka kwa mapigano na kuanzisha mazungumzo ili kutatua masuala ambayo hayajapatiwa muafaka.

Na baadaye siku hiyo ya Jumatano vikosi vya RSF nchini humo vilikubali kusitisha mapigano kwa muda wa saa 24 kuanzia saa kumi na mbili jioni, kufuatia mzozo wa siku nyingi nakugombea madaraka na mapambano ya umwagaji damu na jeshi.

"Tunathibitisha nia yetu ya dhati ya kutaka kusitisha kabisa mapigano, na tunatumaini kuwa upande mwingine utatii usitishaji mapigano kulingana na muda uliotangazwa," RSF iliongeza katika taarifa.

Haikuweza kubainika kwa haraka endapo jeshi lingetangaza msimamo kwake katika usitishaji wa mapigano.

Mahasimu hao walitangaza msimamo wao wa kutaka kusitisha mapigano kwa muda wa saa 24 Jumanne, lakini mwandishi wa shirika la habari la Reuters aliyoko katika mji wa Khartoum alisema alisikia milio ya mizinga ikirushwa baada ya usitishwaji wa mapigano kuanza.

Baadhi ya taarifa zinatoka Shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG