Wakati huo huo, shirika la misaada lisilo la kiserikali Oxfam limeyashutumu makampuni ya kimataifa “kunyakua” maji kutoka nchi masikini kwa kuongeza faida.
Ikitangaza kauli mbiu ya mwaka huu Maji kwa Amani, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba “ wakati maji ni haba au yamechafuliwa au wakati watu hawana fursa sawa au hawana kabisa, mivutano inaweza kuongezeka kati ya jamii na nchi.
“Zaidi ya watu bilioni tatu duniani kote wanategemea maji ambayo yanavuka mipaka ya kitaifa. Wakati ni nchi 24 tu zina makubaliano ya ushirikiano wa maji walio nao” UN imesema. Wakati madadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi ukiongezeka, kuna haja ya haraka ndani ya nchi na kati ya nchi kuungana katika kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu muhimu sana”
Katika jiji kubwa la Johannesburg huko Afrika Kusini, mabomba yamekauka kwa wiki kadhaa, na kuathiri mamilioni ya watu.
Kwenye viunga vya jiji huko Soweto, maelfu ya watu wamekuwa wakipanga foleni kuchota maji katika chupa na ndoo kutoka kwenye matenka yanayoleta maji kutoka nje ya mji huo.
“imekuwa changamoto kubwa, ni wakati wa changamoto kubwa kwa umri wangu ambapo natakiwa niwe hapa kubeba ndoo hizi za lita 20” Thabisile Mchunu mkazi mwenye umri mkubwa zaidi Soweto, aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu. “Cha kuhuzunisha ni kwamba hatujui lini mabomba yetu yatakuwa tena na maji.”
Miundo mbinu inayoporomoka kwa kiasi fulani inalaumiwa uhaba wa maji mjini Johannesburg. Lakini wanasayansi wanasema hali mbaya ya mabadiliko ya hali ya hewa inasababisha kukauka kwa hifadhi huko Afrika kusini na sehemu myingi duniani.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu bilioni 2.2 wanaishi bila udhibiti salama wa maji ya kunywa.
Wanasayansi kutoka jopo la serikali la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa wanasema takribani nusu ya watu duniani wanakabiliwa na uhaba wa maji angalau sehemu ya mwaka, wakati mataifa masikini yaliyoko Kusini mwa dunia yanaathirika zaidi.
Forum