Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 09:45

Osama Bin Laden auwawa


Rais Barack Obama akitangaza kuuliwa kwa kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden nchini Pakistan
Rais Barack Obama akitangaza kuuliwa kwa kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden nchini Pakistan

Rais Barack Obama ametangaza kwamba majeshi ya Marekani yamemuwa gaidi kuu aliyekuwa akisakwa duniani, Osama Ben Laden.

Rais Barack Obama anasema haki imetendeka miaka 10 baada ya mashambulio ya kigaidi dhidi ya New York na Washington Septemba 11, 2001, kutokana na kuuliwa na gaidi kuu aliyekuwa akisakwa zaidi duniani Osama Bin Laden.

Rais Obama amesema Ben Laden aliuliwa ndani ya uwa moja ndani ya Pakistan siku ya Jumapili alipolihutubia taifa kutokea White House.

Majeshi ya Marekani yamekuwa yakimsaka gaidi mkuu kutoka Saudi Arabia tangu mashambulio ya miaka 10 dhidi ya Marekani.

Rais wa Marekani amesema bin Laden hakua kiongozi wa ksilamu , lakini muwaji wa halaiki wa waislamu. Anasema gaidi hiyo alipatikana kutokana na msaada wa ujasusi wa Pakistan.

XS
SM
MD
LG