Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:42

Obama awasili Kenya ijumaa


Mabango ya ukaribisho wa Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Mabango ya ukaribisho wa Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Marekani Barack Obama anaondoka alhamis kwa ziara inayompeleka Ethiopia na Kenya, mahala ambako baba yake mzazi alikozaliwa, huku akielezea umuhimu wa ukuaji wa kiuchumi Marekani akiuhusisha na nchi za kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika.

Atawasili Kenya ijumaa, ambapo atahudhuria mkutano wa Global Entrepreneurship Summit mjini Nairobi. Baadaye ataelekea Ethiopia na kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kutembelea nchi hiyo.

Makundi ya haki za binadamu yanaikosoa ziara ya bwana Obama kwenda Ethiopia kwa sababu namna nchi hiyo inavyoshughulikia masuala yake ya kisiasa.

Jumatano jioni bwana Obama alizungumza kuhusu biashara na bara la Afrika kwenye tafrija huko White House akiadhimisha utiaji saini wa mkataba wa biashara wa Afrika na Marekani, African Growth and Opportunity Act (AGOA). Alisema licha ya changamoto katika bara la Afrika, Afrika ni mahala penye mabadiliko na kuna masoko yanayokuwa kwa kasi duniani. Alisema bara lina nafasi ya kuwa kiini kijacho cha fursa ya kiuchumi ulimwenguni.

Alisema sheria ya biashara itaendelea kuhamasisha utawala bora, haki za wafanyakazi na haki za binadamu barani Afrika.

Mabao ya ukaribisho wa Obama.
Mabao ya ukaribisho wa Obama.

Bwana Obama mwezi uliopita alitia saini kuongeza kwa miaka 10 zaidi mamlaka ya biashara nchini na bara la Afrika, juhudi za miaka 15 ambazo ziliboresha biashara ya Marekani na Afrika kufikia dola bilioni 73 mwaka jana na Marekani. Mauzo ya nje ya bidhaa yaliongezeka kwa kiasi kidogo ya nusu kwa jumla.

Zaidi ya mataifa 40 ya kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika yanastahili faida za biashara chini ya sheria hiyo kupitia uagizaji bidhaa zaidi kutoka Afrika kuingia Marekani bila ya kutozwa ushuru. Maeneo mawili makuu yanayonufaika sana ni wauzaji wa mafuta nje ya nchi, Angola na Nigeria.

XS
SM
MD
LG