Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:45

Rais Kenyatta ahutubia taifa juu ya ujio wa Rais Obama


Rais Uhuru Kenyatta, (R) akiwa na Naibu Rais wake, William Ruto, akihutubia ujio wa Rais Obama, Nairobi, July 21, 2015.
Rais Uhuru Kenyatta, (R) akiwa na Naibu Rais wake, William Ruto, akihutubia ujio wa Rais Obama, Nairobi, July 21, 2015.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alilihutubia taifa jumanne kuhusu ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama anayetarajia kutembelea huko mwishoni mwa wiki.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akiwahutubia waandishi wa habari katika ikulu ya Nairobi kuhusu ziara hiyo Rais Uhuru Kenyatta amezungumza kwa kirefu kuhusu mkutano ujao wa wajasiliamali mjini Nairobi pamoja na mazungumzo yake na Rais Obama kuhusu uhusiano wa nchi hizi mbili. Lakini alipoulizwa maswali na waandishi wa habari juu ya masuala ya ndoa za jinsia moja na haki za mashoga, Rais Kenyatta alisema mambo hayo sio muhimu.

Rais Uhuru Kenyata
Rais Uhuru Kenyata

Rais Kenyatta alisema “umuhimu wa ziara ya Rais Obama ni kuimarisha uhusiano wa Kenya na nchi ya Marekani. Umuhimu wa ziara hii haswa ni kuhimiza mambo ya uchumi na vile tunaweza kuendelea kuimarisha biashara ya pamoja na nchi hiyo. Sasa sana pia hii ni nafasi kwetu sisi kufungua milango yetu kuonesha yale ambayo tumeweza kutenda ndio tuweza kuimarisha jinsi biashara inafanywa katika nchi yetu na kuwafungulia milango wawekezaji kutoka nchi ya Amerika na pia kutoka nchi zingine waweze kuja waweke mali zao hapa waweze kupanua kama ni viwanda na mambo mengine na mambo haya ndio yatatusaidia kuhakikisha kwamba tumeweza kuajiri vijana wetu ambao wanahitaji kazi pia kuweza kuhimiza urafiki katika mambo kama vile ya IT ambapo vijana wetu wameonesha ujuzi kweli kweli ni kwa njia gani wanaweza kushirikiana na makampuni mengine ya nchi za nje ndio waweze kupanua biashara zao.

Vile vile Rais Kenyatta alisema mazungumzo yake yatagusia tatizo kubwa la kitisho cha ugaidi na kitisho cha mabadiliko ya hali ya hewa.

XS
SM
MD
LG