Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 10:56

Kenya, Ethiopia wafanya mashambulizi Somalia.


Wanajeshi wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia kwenye picha ya awali.
Wanajeshi wa Kenya karibu na mpaka wa Somalia kwenye picha ya awali.

Kabla ya ziara ya Rais Barack Obama kutembelea Afrika Mashariki, ambayo inaanza baadaye wiki hii, wanajeshi wa Kenya na Ethiopia wanaofanyia operesheni zao nchini Somalia wameanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab katika mikoa ya Gedo na Bay.

Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, kinachojulikana kama AMISOM, kimetangaza mashambulizi “Operation Juba Corridor” na kusema yanalenga kuling’oa kundi la kigaidi kutoka maeneo ya vijijini.

Awamu ya kwanza ya mashambulizi hayo mawili ilifanywa Ijumaa kutokea Fafahdhun, kituo cha kijeshi kinachoendeshwa na wanajeshi wa Kenya kutokea mkoa wa Gedo. Wanajeshi siku ya Jumapili wamefika Tarako, kiasi cha kilometa 50 magharibi mwa mji wa Bardhere. Ni shambulizi la mwisho kubwa kwa ngome ya Al Shabab katika mkoa wa Gedo.

Shambulizi la pili lilifanywa Ijumaa kutokea mji wa Qasanhdhere katika mkoa wa Bay na lilifanywa na wanajeshi wa Ethiopia na serikali ya Somalia. Wanajeshi hao wamefika Esow, kiasi cha kilometa 65 kaskazini mwa Bardhere, kwa mujibu wa Omar Sheikh Ismail, msemaji wa majeshi ya Somalia yanayopigana sambamba na wanajeshi wa Ethiopia.

Pia ameiambia VOA kwamba operesheni hiyo imehusisha matumizi ya ndege.

Wanajeshi wa Ethiopia pia wanatarajiwa kushambulia Dinsor, makao makuu ya muda ya Al Shabab, lakini operesheni hiyo imekutana na upinzani kwa mujibu wa mwandishi wa VOA aliyeko Baidoa.

XS
SM
MD
LG