Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:16

Nigeria : Watu 50 wauawa katika vijiji kadhaa jimbo la Kaduna


Wanajeshi wa Nigeria wakiweka kizuizi sehemu ambayo mtu mmoja inashukiwa aliuawa na wanamgambo katika kitongoji cha Polo enoe la Maiduguri, Nigeria February 16, 2019. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Wanajeshi wa Nigeria wakiweka kizuizi sehemu ambayo mtu mmoja inashukiwa aliuawa na wanamgambo katika kitongoji cha Polo enoe la Maiduguri, Nigeria February 16, 2019. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo

Majambazi yenye silaha yameua watu wasiopungua 50 katika vijiji kadhaa vilivyoko katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria Jumapili, kwa mujibu wa maelezo ya polisi na wakazi wa eneo hilo.

“Idadi hiyo siyo ya mwisho kuna uwezekano ikaongezeka kadiri juhudi za uokoaji zinavyoendelea,” Zayyad Ibrahim, mbunge nchini Nigeria ameliambia shirika la wakala wa habari la Ufaransa (AFP) Jumatatu.

Majambazi hao walianza kufyetua risasi kila upande, wakati waumini wakitoka msikitini baada ya sala ya alfajiri, Ibrahim amesema, akiongeza kuwa waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali mbili zilizoko katika eneo.

Dayyabu Kerawa, diwani katika eneo, amesema mashambulizi hayo yamefanyika kulipiza kisasi operesheni ya jeshi inayofanywa dhidi ya majambazi hao katika eneo. Washambuliaji hao “wamewatuhumu wakazi wa vijiji hivyo kwa kutoa taarifa zao mahali walikojificha kwa jeshi hilo,” amesema.

According to local police, about a hundred armed men attacked the villages of Kerawa, Rago,Zareyawa, Marina, Hashimawa, and Unguwar Barau, all in the Igabi district, shooting residents, and looting and burning homes.

Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, takriban watu mia moja wenye silaha walivamia vijiji vya Kerawa, Rago, Zareyawa, Marina, Hashimawa, na Unguwar Barau, ambavyo vyote viko katika wilaya ya Igabi, na majambazi hao walipiga bunduki na kuiba pamoja na kuchoma nyumba za wakati hao.

Last month 21 people, 16 of them belonging to one family, were killed in killed in similar attacks on the village of Bakali in the neighboring Giwa district.

Mwezi uliopita watu 21, kumi na sita kati yao wakiwa wanafamilia moja, waliuawa katika mashambulizi kama hayo katika kijiji cha Bakali jirani na wilaya ya Giwa.

XS
SM
MD
LG