Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:41

Watoto takriban 50 waokolewa baada ya jengo la ghorofa kuanguka Nigeria


Shughuli za uokoaji zikiendelea Alhamisi mjini Lagos, Nigeria baada ya jengo la ghorofa kuporomoka, Jumatano, Machi 14, 2019
Shughuli za uokoaji zikiendelea Alhamisi mjini Lagos, Nigeria baada ya jengo la ghorofa kuporomoka, Jumatano, Machi 14, 2019

Watoto takriban 50 wameokolewa baada ya jengo kuporomoka katika kitongoji Itafaji mjini Lagos, na hivi sasa wanapatiwa matibabu katika hospitali moja nchini humo.

Serikali ya Nigeria wamethibitisha kuwa baadhi ya watu walipoteza maisha bila ya kutaja idadi yao. Jengo hilo la ghorofa nne ambapo kulikuwa na shule, makazi ya watu, na maduka. Jengo hilo lilianguka siku ya Jumatano.

Wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa shule hiyo ilikuwa na watoto takriban 100. Wakoaji walikuwa wanajaribu kutafuta daftari lililokuwa na majina ya watoto waliosajiliwa katika shule hiyo, ili kupata idadi ya watoto waliokufa katika ajali hiyo, afisa wa uokoaji ameiambia VOA.

Watoto walikuwa ndani ya jengo

Ajali hiyo ilitokea majira ya alfajiri saa kumi kasoro dakika 10, saa za Nigeria, wakati watoto wakiendelea na masomo.

Majirani hapo awali walifanya juhudi za kuwaokoa watu kutoka katika kifusi kabla kikosi cha waokoaji kuwasili na kujiunga nao wakileta mitambo yakuharakisha uokoaji wa watu kutoka eneo la ajali.

Gavana wa Jimbo la Lagos Akinwunmi Ambode alipowasili alisema: "unajua tukiwa tuna shughulikia aina hii ya kazi ya kuwaokoa watu, wengi hukusanyinka kujiunga na shughuli hii. Lakini, ninataka kuwaambia kwamba ina lazimu kutoa nafasi kwa wafanyankazi wa uokoaji kutekeleza wajibu wao. Hapa Itafaji, huu sasa ni mfano mkubwa na wakati tunapo endelea na zoezi la kutathmini kila jengo, … tutabomoa nyumba hatarishi na watu watahamishwa kwa haraka..."

Mkurugenzi wa shirika la uokoaji

Naye Mkurungezi wa Shirika la Uokoaji, Adesina amesema : “Tume waokoa watu, na unajua watu waliojeruhiwa wanaweza kufa badaaye hospitalini. Lakini tume waokoa watoto kama 60 na watu wazima kama watatu. Bahati ni kwamba kuna hospitali mbili karibu na eneo hilo la ajali. Hospitali Kuu ya Lagos na hospitali ya watoto. Lakini mpaka kazi itakapomalizika, hivi sasa sitaweza kusema idadi halisi ya waliopoteza maisha au walioathiriwa na ajali hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Nigeria, jengo hilo la ghorofa lililoanguka ni kongwe na linatakriban miaka 30 tangu kujengwa. Zoezi la bomoabomoa linaendelea katika eneo hilo chini ya mpango wa serikali wa kujenga nyumba za kisasa na kuboresha mazingira.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Collins Atohengbe, Nigeria

XS
SM
MD
LG