Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:48

Niger: Kiongozi wa zamani wa uasi na mwanasiasa aanzisha harakati za kuupinga utawala wa kijeshi


Rhissa Ag Boula (VOA/Nicolas Pinault)
Rhissa Ag Boula (VOA/Nicolas Pinault)

Kiongozi wa zamani wa uasi na mwanasiasa wa Niger ameanzisha vuguvugu kuupinga utawala wa kijeshi uliochukua madaraka julai 26 kwa njia ya mapinduzi , ikiwa ni ishara ya kwanza kuupinga utawala wa kijeshi katika nchi hiyo ya kimkakati kwenye eneo la Sahel.

Rhissa Ag Boula amesema katika taarifa iliyoonekana leo, kwamba baraza lake jipya la upinzani kwa jamhuri – CRR linalenga kumrejesha madarakani rais Mohamed Bazoum ambaye yuko katika kizuizi nyumbani kwake tangu jeshi lichukue madaraka.

Niger ni muathirika wa janga lililoratibiwa na watu waliopewa dhamana ya kuilinda, ilisema taarifa hiyo.

kuanzishwa kwa vuguvugu hilo kunakuja wakati ambapo juhudi za kidiplomasia za kubadili mapinduzi zimekwama baada ya utawala wa kijeshi kuukataa ujumbe wa karibuni kabisa na serikali za kijeshi za nchi jirani Mali na Burkina Faso ambazo zinaunga mkono mapinduzi hayo zikitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuzuiya uingiliaji wowote wa kijeshi.

Viongozi wa mapinduzi wa Niger wameukatalia ujumbe wa Afrika na umoja wa mataifa kuingia nchini humo siku ya jumanne, wakipinga shinikizo la mashauriano kabla ya Mkutano wa kilele hapo kesho ambapo wakuu wa nchi za jumuiya ya kiuchumi ya afrika magharibi – Ecowas kuwa watajadili uwezekano wa matumizi ya nguvu.

Forum

XS
SM
MD
LG