Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:30

Kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi ya Niger lakataa kushauriana na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na kieneo


Wafuasi wanaounga mkono mapinduzi ya kijeshi ya Niger wakiwa kwenye mkutano mjini Niamey. Agosti 6, 2023
Wafuasi wanaounga mkono mapinduzi ya kijeshi ya Niger wakiwa kwenye mkutano mjini Niamey. Agosti 6, 2023

Kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi ya Niger limekataa juhudi za hivi karibuni zaidi za kidiplomasia za kumrejesha madarakani rais aliyeondolewa, Muhamed Bazoum.

Kundi hilo limepinga ziara iliyopangwa na wawakilishi wa jumuiya ya kieneo ya ECOWAS, Umoja wa Africa na Umoja wa Mataifa Jumanne, kulingana na barua iliyoonekana na shirika la habari la AP.

Barua hiyo ilitaja kile ilichokieleza kama “sababu zilizo wazi za kiusalama katika mazingira ya uhasama” dhidi ya Niger wiki mbili, baada ya kundi la kijeshi kufanya mapinduzi nchini humo, na kuondoa rais aliyechaguliwa kidemokrasia. ECOWAS ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo kundi hilo halingeresha rais Mohamed Bazoum kufikia Jumapili, lakini hilo halikufanyika.

Jumatatu kaimu naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Victoria Nuland alikutana na baadhi ya viongozi wa mapinduzi ambao hawamkuruhusu kukutana na rais aliyeondolewa madarakani. Alisema kwamba mafisa hao hawakuonekana kuwa na ari ya kuanza mashauriano yoyote kuelekea kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba. Rida Lyammouri ambaye ni mmoja wa viongozi kwenye kituo cha Sera cha New South amesema kwamba mbinu za kidiplomasia za Washington hazilengi kuhujumu zile za ECOWAS.

Forum

XS
SM
MD
LG