Niger iliwekewa vikwazo zaidi siku ya Jumanne saa chache baada ya viongozi wake wapya wa kijeshi kukataa ujumbe wa hivi karibuni wa kidiplomasia unaolenga kurejesha utulivu wa kikatiba kufuatia mapinduzi ya Julai 26.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliamuru vikwazo hivyo vipya kupitia benki kuu ya Nigeria vinavyolenga kuwabana waliohusika katika utwaaji huo msemaji wa rais alisema.
Vikwazo hivyo viliwekwa baada ya serikali kuu kukataa ujumbe wa pamoja kutoka mataifa ya Afrika Magharibi, Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa ruhusa ya kuingia Niger kupinga shinikizo la Marekani na Umoja wa Mataifa kuja kwenye meza ya mazungumzo
Usiku wa Jumanne Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilithibitisha kuwa ujumbe huo wa pamoja umesitishwa na kusema katika taarifa yake itaendelea kupeleka hatua zote ili kurejesha utulivu wa kikatiba nchini Niger.
Forum