Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:08

Niger: EU, Marekani zawataka wanajeshi waliokamata madaraka kumrejesha Bazoum katika uongozi


FILE - Niger President Mohamed Bazoum at the presidential palace in Niamey, Niger, March 16, 2023.
FILE - Niger President Mohamed Bazoum at the presidential palace in Niamey, Niger, March 16, 2023.

Umoja wa Ulaya na Marekani zimewataka wanajeshi waliokamata madaraka nchini Niger wiki iliyopita kusitisha mapinduzi na kumrejesha Rais Mohamed Bazoum katika uongozi.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell siku ya Jumatatu ameeleza kuunga mkono hatua zilizochukuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambapo siku ya Jumapili waliwawekea vikwazo viongozi wa mapinduzi na kuwapa wiki moja kuachia madaraka au watakabiliwa na hatua ikiwemo “matumizi ya nguvu.”

Borrell alisema katika taarifa kuwa Bazoum lazima arejeshwe madarakani bila ya kuchelewa.

Josep Borrell
Josep Borrell

Pia alisema kuwa EU inapinga tuhuma za mataifa ya nje kuingilia kati na itawawajibisha viongozi hao wa kijeshi kwa vitendo vyovyote vya kuwashambulia raia au dhidi ya wafanyakazi wa kidiplomasia au majengo yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken pia alikaribisha kile alichokiita uongozi imara wa ECOWAS katika “kutetea utaratibu wa kikatiba nchini Niger” alisema Marekani inaungana na wito wa kuachiwa mara moja Bazoum na kuirejesha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Antony Blinken
Antony Blinken

Viongozi wa mapinduzi wamesema walifanya mapinduzi wiki iliyopita kujibu kile walichokieleza hali mbaya ya usalama nchini Niger na serikali kutochukua hatua dhidi ya wana jihadi wa Kiislam.

Katika taarifa kupitia televisheni ya taifa Jumatatu, viongozi hao wa kijeshi wameushutumu utawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa kutaka kutumia hatua za kijeshi kumkomboa Bazoum.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG