Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:53

Viongozi wa Afrika waupa utawala wa kijeshi nchini Niger wiki moja kuachia madaraka


Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, wa pili kutoka kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Afrika Magharibi baada ya mkutano mjini Abuja Nigeria, Jumapili, Julai 30, 2023. (AP)
Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, wa pili kutoka kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Afrika Magharibi baada ya mkutano mjini Abuja Nigeria, Jumapili, Julai 30, 2023. (AP)

Katika mkutano wa dharura Jumuiya ya ECOWAS imetaka Bazoum arejeshwe madarakani vinginevyo utachukua hatua zote kurejesha utaratibu wa Kikatiba

Viongozi wa kiafrika siku ya Jumapili waliupa utawala wa kijeshi nchini Niger wiki moja kuachia madaraka au kukabiliana na uwezekano wa matumizi ya nguvu na kuwawekea vikwazo vya kifedha waasi baada ya mapinduzi ya hivi karibuni katika eneo la Sahel linalokumbwa na wanajihadi na kuzusha wasiwasi katika bara hilo na nchi za Magharibi.

Katika mapinduzi ya tatu ndani ya miaka mingi ya kuangushwa kwa kiongozi katika eneo la Sahel rais wa Niger aliyechaguliwa kidemokrasia na mshirika wa Magharibi Mohamed Bazoum amekuQ akishikiliwa na jeshi tangu siku ya Jumatano.

Jenerali Abdourahamane Tiani mkuu wa kikosi chenye nguvu cha walinzi wa rais amejitangaza kuwa kiongozi.

Bazoum ni mmoja wa kundi la marais waliochaguliwa ambao idadi yao inapungua na wanaounga mkono nchi za Magharibi katika eneo la Sahel ambako tangu mwaka 2020 wanajihadi wameanzisha mapinduzi nchini Mali na Burkina Faso.

Mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa na Umoja wa Ulaya wamesitisha ushirikiano wa kiusalama na msaada wa kifedha kwa Niger kufuatia mapinduzi hayo huku Marekani ikionya kuwa msaada wake pia unaweza kuwa hatarini.

Katika mkutano wa dharura nchini Nigeria Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilitaka Bazoum arejeshwe madarakani ndani ya wiki moja.

Vinginevyo umoja huo ulisema utachukua hatua zote kurejesha utaratibu wa Kikatiba.

Forum

XS
SM
MD
LG