Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:59

AU na EU zinataka jeshi la Niger kurejesha mamlaka ya kikatiba ndani ya siku 15


Jenerali Abdourahmane Tchiani akitoa taarifa kwenye television ya taifa Ijumaa. July 28, 2023, Niamey, Niger.
Jenerali Abdourahmane Tchiani akitoa taarifa kwenye television ya taifa Ijumaa. July 28, 2023, Niamey, Niger.

Jenerali Abdourahamane Tiani mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais tangu mwaka 2011 alionekana kwenye televisheni ya taifa siku ya Ijumaa akijitangaza kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, iliyo na matatizo

Umoja wa Afrika (AU) umelitaka jeshi la Niger kurejea kwenye kambi zao na kurejesha mamlaka ya kikatiba ndani ya siku 15 huku Umoja wa Ulaya (EU) pia ukiongeza shinikizo Jumamosi kwa viongozi wa mapinduzi ikisitisha ushirikiano wa kiusalama na nchi hiyo inayotaabika na ghasia za wanajihadi.

Jenerali Abdourahamane Tiani mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais tangu mwaka 2011 alionekana kwenye televisheni ya taifa siku ya Ijumaa akijitangaza kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, iliyo na matatizo.

Vikosi vyake vimemfungia Rais Mohamed Bazoum aliyechaguliwa kidemokrasia kwenye makazi yake rasmi katika mji mkuu wa Niamey tangu Jumatano, katika hatua ambayo Tiani amewasilisha kama jibu la kuyumba kwa hali ya usalama inayohusishwa na umwagaji damu wa kijihadi.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya wameungana kulaani vikali unyakuzi wa madaraka unaokemewa kimataifa ikiwa ni hatua ya hivi karibuni kulikumba eneo la Sahel.

Forum

XS
SM
MD
LG