"Tunasisitiza kwa matamshi makali sana ya wazi ya jumuiya ya kimataifa ya kutaka kurejeshwa mara moja taratibu za kikatiba na mamlaka ya kidemokrasia yaliyochaguliwa ya kiraia” wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa yake.
Mlinzi wa rais, Jenerali Abdourahamane Tiani, alionekana katika kituo cha televisheni ya taifa Ijumaa akitetea mapinduzi ya wiki hii, akirudia kuwa askari walikuwa wamechukua hatua hiyo kulinda usalama wa taifa.
Mlinzi huyo alimzuia Rais Mohamed Bazoum ikulu Jumatano. Baadaye kundi la maafisa walionekana kwenye televisheni ya taifa wakisema kuwa wamevua madaraka Bazoum.
Usalama bado ni tatizo tangu Bazoum aingie madarakani mwaka 2021 wakati wanajihadi ambao walikita mizizi katika nchi jirani ya Mali mwaka 2012 walipopata nguvu nchini humo, na kuua maelfu na kusababisha zaidi ya watu milioni sita kote kukoseshwa makazi kote katika eneo la Sahel huko Afrika Magharibi.
Niger ni mshirika mkuu wa nchi za Magharibi katika kukabiliana na uasi wa Kiislamu huko Afrika Magharibi na uwepo wa idadi ya wanajeshi kutoka mataifa ya kigeni yakiwemo ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa.
Rais wa ufaransa, Emmanuel Macron alisema yuko tayari kuunga mkono vikwazo dhidi ya wahusika wa mapinduzi "hatari", baada ya waziri wake wa mambo ya nje kusema unyakuzi wa mamlaka hauonekani kuwa wa uhakika.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters
Forum