"Marekani ndiyo demokrasia kongwe zaidi, na India ndiyo demokrasia kubwa zaidi," Modi alisema, akihutubia kikao cha pamoja cha bunge la Marekani.
"Ushirikiano wetu unadhihirisha vyema mustakabali wa demokrasia, " alisema.
Wabunge hao walisifu hotuba ya Modi kama fursa muhimu ya kuunda uhusiano wa karibu kati ya Marekani na India, hata kama bado kuna wasiwasi juu ya rekodi ya haki za binadamu ya Modi.
Modi aliwaambia wabunge hao kwamba uchumi unaokua kwa kasi wa India ulitokana na maendeleo yanayoongozwa na wanawake na uvumbuzi wa kiteknolojia wa kizazi kipya.
"Ninatazamia kuongezeka kwa uhusiano wa kiuchumi na usalama wa kitaifa kati ya mataifa yetu mawili makubwa,” Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy alisema katika taarifa kufuatia hotuba hiyo.
Forum