Dorsey ambaye aliondoka kwenye wadhifa wa kuongoza Twitter 2021, amesema pia kwamba India imetishia kufanya msako dhidi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo iwapo hawataondoa taarifa walizoagizwa kuondoa kwenye mtandao huo.
Naibu waziri wa habari na teknolojia wa India Rajeev Chandrasekhar pia amejibu madai ya Dorsey akisema kwamba ni ya uongo. Matamshi ya Dorsey yameibua mjadala mkali wa kimataifa kutokana na kuwa ni nadra kwa makampuni ya kimataifa nchini India kukosoa serikali moja kwa moja.
Dorsey ameongeza kwamba Twitter pia imetishiwa na serikali za Uturuki na Nigeria, ambako huduma zake zilisitishwa kwa muda kabla ya kurejeshwa tena.
Forum